Saturday, 27 July 2013

DENTI ANASWA UCHAWI.

                                                
Stori:Gladness Mallya na Haruni Sanchawa

AMINI usiamini, duniani kuna uchawi! Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Pasco (21) ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Samaritan iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara amekutwa getini kwa kaka’ke, Edward Raphael akiwa amefungwa kamba na matunguri.
Denti akiwa amaefungwa kamba
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni huko Yombo-Buza jijini Dar na kuibua sekeseke la aina yake kutokana na mazagazaga ya kichawi aliyokutwa nayo. Kwa mujibu wa mashuhuda kijana huyo alikuwa  amefungwa kamba miguuni na mikononi, huku akiwa na nguo za ndani pekee.
Na pia habari hizo zimeongeza kuwa Pasco alikuwa amepakwa unga na kuandikwa maneno ya kiarabu mwilini, huku kiunoni akiwa na shanga, jambo ambaloliliwashangaza wengi.
 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!