Friday 26 July 2013

MUME NA MKE WAUA MTOTO WAO WAKATI WAKIGOMBANA NDANI.....BAADA YA KUUA, MTOTO ATUPWA KWA JIRANI YAO


 
Polisi mkoani Rukwa inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wao wakati wanapigana kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa polisi Mkoa Rukwa, Jacob Mwarwanda amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Julai 22, saa 5:30 za usiku baada ya Livinus Choma(31) na mkewe  Grace Choma(28) ambao wote wakazi wa Malangali kugombana usiku.

Amesema baada ya mume na mke kurejea nyumbani ulizuka ugomvi baina yao huku mwanamke akimtuhumu mume wake kwamba anauhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine na kusababisha waanze kupigana.

Wakiwa wanapigana ghafla mume alimsukuma mke wake ambapo alitereza na kuanguka kitendo kilichosababisha kumlalia mtoto wao aitwaye Esther choma(2)  ambaye alipoteza fahamu hali ambayo wazazi hao walijua wamemuua mtoto wao huyo.

Baada ya mtoto kupoteza fahamu wanandoa hao walichukua mwili wa mtoto huyo na kwenda kuutelekeza katika nyumba ya jirani yao na kisha kupiga simu kwa diwani wa kata hiyo wakidai kuwa mtoto wao amepotea katika mazingira ya kutatanisha

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!