Friday 26 July 2013

HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL

 


KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe.


Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt.

Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.
 
 “Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai.


Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini anafaidi sana  kuwa na mwanaume huyo.







 


Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!