MEMBA wa zamani wa kundi la Destiny’S Child, Kelly Rowland ameokolewa kuzama katika pwani ya Massachusetts Ijumaa iliyopita baada ya boti waliyokodi kusukumwa mbali nje ya bahari.
Staa huyo wa nyimbo kali za ‘Survivor’ na 'Dirty Laundry' alikuwa katika safari ya kutalii akiwa na jamaa zake wengine wanne wakati boti yao ilipopoteza mwelekeo kutokana na upepo mkali na nahodha kulazimika kuwapigia simu walinzi wa pwani katika hifadhi ya taifa ya baharini ya Stellwagen kuomba msaada.
Maofisa hao wa usalama baadae jioni walimsindikiza Rowland na wenzake hadi kwenye mji wa Provincetown, na kwa mujibu wa gazeti la Wicked Local, mwimbaji huyo na rafiki zake walikuwa salama.
Kwa mujibu wa mtandao wa jarida la UsMagazine, Rowland aliweka nyuma matatizo hayo siku iliyofuata na kuingia madukani kufanya manunuzi kwa ajili ya zawadi
No comments:
Post a Comment