Tuesday 23 April 2013

RUFAA YA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ABDALLA ZOMBE NA WENZAKE YATUPILIWA MBALI.





Mahakama ya Rufani Tanzania imekwama kusikiliza rufaa ya Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane baada ya kubaini kuwapo kwa kasoro kwenye taarifa ya rufaa hiyo

Kutokana na hali hiyo Jamhuri imeomba iruhusiwe kufanya marekebisho, lakini upande wa utetezi umepinga na kuiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo.

Baada ya upande wa utetezi kutoa msimamo huo sasa mahakama hiyo itatoa uamuzi siku nyingine.

Rufaa hiyo iliyokatwa na Serikali kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe na wenzake, inatarajiwa kusikilizwa mfululizo.

Katika rufaa ya Zombe, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), ilikata rufani kupinga hukumu ya kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa mkoani Morogoro na dereva teksi iliyokuwa ikimkabili Zombe na wenzake.


Haikuelezwa ni lini shauri hilo litasikilizwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!