Wednesday 24 April 2013

BINTI AFUNGUKA ADAI AMEWAAMBUKIZA WANAUME WENGI VIRUSI VYA UKIMWI.


Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote usifute hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.

Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge


Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu

Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu

Mwisho nawashauli wababa kuridhika na wake zao na wamama pia ridhikeni na waume zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko unavyozani.


Habari kwa hisani ya mpekuzi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!