Friday 29 March 2013

HAYA JAMANI NAFASI ZA KAZI HIZO


Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.

Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.  27 Machi, 2013

Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975  
Mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!