Saturday 15 May 2021

HOMONI YA PROLACTIN KUPANDA KWA MWANAMKE SIO ISHARA NJEMA

 


Ninacho kiona ni kwamba ni rahisi sana mwanamke chini ya miaka 30 kubeba mimba kwa urahisi kuliko miaka zaidi ya 30. Yaani Binti wa miaka 20-25 mimba ni Gusa Unase inaingia bila msaada wa daktari. Ila umri kadri unavyozidi kwenda Uwezekano huo Unakuwa mdogo sana mpaka Daktari aingilie kati Akubadilishie baadhi ya vitu ndipo Mimba iingie.

Wanawake wengi hili tatizo ni Kubwa sana. Ninadhani ni Kutokana na vyakula na mifumo yetu ya maisha ya kila siku. Ina maana kadri unavyozidi kuponda raha ya Vyakula ndivyo Hali ovari zako zinavyo sinzia.
.
Homoni ya Prolactin kawaida Gusa unase mimba inatakiwa isome kwenye sanu chini ya 15ng/ml ina inaruhusiwa kupanda na isizidi 24ng/ml. Ina maana Kadri inavyozidi kupanda Ina ashiria kuna Vitu Vina Endelea Vinavyo UDHURU MWILI WAKO NA UGUMU WA KUPATA MIMBA UNAONGEZEKA.
.
Homoni hii husaidia Kukuza matiti wakati wa mimba na kuzalisha maziwa wakati unanyonyesha. Lakini inapopanda wakati haupo kwenye nyakati hizo ina ashiria Ugonjwa tunaita Hyperprolactinemia. Hali hii usababisha maumivu makali ya hedhi, Dalili mbaya kabla ya hedhi na ndani ya hedhi, Kutokwa damu nyingi, Kuingia hedhi zaidi ya mara moja ya mwezi kuota ndevu kukosa hamu ya tendo na ndoa, Kuwa mkavu sana wakati wa tendo na mwisho kutokwa maziwa kwenye chuchu.
.
MAMBO YANAYO SABABISHA PROLACTIN KUWA JUU
1. KITAMBI NA UZITO MKUBWA
Kadri unavyo ongeza hazina ya mafuta unaongeza chanzo cha uzalishaji wa homoni ya Estrogen kutoka kwenye seli zinazo hifadhi mafuta. Tukio hili hupandisha Prolactin. Hivyo Punguza Kitambi Usije Hangaika Kusaka Mtoto kwenye ndoa hapo baadae.
2. Magonjwa ya Tezi ya Thyroid. Endapo tezi ya shingo ikianza kuzalisha homoni chini ya kiwango salama kwa sababu ya Maradhi km Hashimoto's nk. Ugonjwa huu Huchochea uzalishaji wa Thyrotropin Releasing Hormones kwa Wingi ambayo hupandisha PROLACTIN.
3. Kutokupevusha Yai. Mwanamke unaweza kuingia hedhi lakini Yai halijapevuka. Unayeingia siku chache au Nyingi. Hali hii Huchochea Gonadotropin Releasing Homoni kutemwa kwa wingi na hupandisha Prolactin. Ina maana ukikuta prolactin iko juu moja ya sababu ni HUPEVUSHI MAYAI.
4. Magonjwa ya Uvimbe katika seli Zinazotema Prolactin katika Ubongo Prolactinoma. Hasa kwa wale prolactin ikiwa iko zaidi ya 100ng/ml. Lazima ufanyiwe uchunguzi zaidi kwenye Bakuli linalobeba tezi ya Pituitary tunaita Sella turcica kwa kutumia Picha za Ungo za MRI au CT scan.
5. Kupanda kwa Homoni za Ukuaji yaani Growth Hormones. Sayansi inaonesha kwamba kutawala kwa homoni za ukuaji katika damu kuna athiri homoni ya maziwa kwa sababu ya Kuongezeka kwa Kichocheo kiitwaho Growth hormone Releasing homoni ambayo husisimua tezi za Idara ya chini Kutoa homoni za ukuaji.
6. Msongo wa mawazo. Hili husababisha Tezi hii Kutema homoni nyingi kwa sababu ya kuongezeka kwa Adrenocorticotrophic Hormone (ACTH) ambayo huongeza uzalishaji wa Homoni za msongo cortisol kutoka kwenye tezi ya adrenali. Ingawaje kupanda kwa homoni ya Prolactin kwa sababu ya mawazo huwa haidumu mara nyingi pia huwa haiwezi kuzidi 24ng/ml.
7. Maradhi ya Kisukari, Mazoezi magumu ya Kimashindano ya Marathon, ambayo Unaenda kushindana ili upate medali. Mwanamke unaweza kupitia hii changamoto kwa sababu ya tension kali ya mashindano hayo.
8. Vyakula hasa vyakula vya wanga na sukari. Tafiti zinaonesha kwamba kiwango cha Prolactin hupanda kwenye damu kwa kuathiriwa na kupanda kwa homoni Inayotolewa na utumbo mwembamba iitwayo Vasoactive Intestinal Peptide (VIP). Homoni hii hupanda baada ya chakula kuingia kwenye utumbo mwembamba. Ndio maana ni vizuri zaidi Unaushauriwa Kupima Homoni hii Asubuhi Ukiwa hujala chochote na hujapitia misuko suko ya maisha utapata jibu zuri zaidi lenye uhalisia.
Pia unashauriwa Homoni hii Upime baada ya Kupevusha mayai kwa sababu hormoni kutoka kwenye Ubongo iitwayo Gonadotropin Releasing hormone huwa ipo chini na ikiwa juu hupandisha homoni ya Prolactin. Hivyo baada ya Kupevusha yai homoni hio huwa ipo chini katika Kipindi cha Luteal phase hivyo utapata pia Jibu zuri.
.
Wanawake wengi Homoni hii haipo vizuri na Inawatesa kwa kuwakosesha hamu ya tendo la Ndoa na Kuvuruga Homoni. Badala ya kutatua tatizo wanakimbilia uzazi wa mpango kwa sababu wanashindwa kupanga uzazi kwa kalenda sababu mzunguko haueleweki kwa sababu homoni hii imevuga homoni na Imekaba roba ovari hazipevushi mayai.
Kabla ya kushughulikia Jambo Lolote la uzazi HOMONI HII LAZIMA ICHUNGUZWE NA ISHUGHULIKIWE.
Una Maoni Kuhusu Makala Hii? Usikose KITABU CHANGU CHA SAYANSI YA HOMONI NA UGUMBA SIKU SIO NYINGI KITATOKA UTAKISOMA NA NINA MATUMAINI UTAKIFURAHIA

Dr. Boaz Mkumbo MD


3 comments:

Anonymous said...

Naomba nisaidie prolactin ipo juu

Sophie mbeyu said...

Muone huyo Dr hapo chini nimekuwekea. Dr. Boaz Mkumbo MD

Anonymous said...

Ni dawa gani utatumia km una huo ugonjwa

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!