Saturday 15 May 2021

Anaandika Dinamarious!

 
“Amani ya moyo......Amani ya moyo hailetwi na mtu usimtegemee mtu kukupa amani ya moyo.Tena mtu anaweza kukudisapoint hisia za mtu zinaweza kubadilika muda wowote.Aliyekupa raha huyo huyo akakupa maumivu na uchungu mwingi.


Amani ya moyo hailetwi na vitu eti labda huo mshahara ukipanda kazini utakuwa na raha na amani,ukipata pesa,ukijenga nyumba,ukinunua gari,ukiolewa,ukioa, hakuna kitu kama hicho.Always always changamoto zipo na ndio dunia inavyokwenda.Kubwa tafuta amani ya moyo....kujikubali,kukubali maisha yako,kujipa muda wa kufanikisha jambo flani kuwa ni process sio kufumba na kufumbua.
.
Usitamani maisha ya wengine au mafanikio yao yakakunyima usingizi.Kukubali kuwa jambo flani limeshindikana angalia plan B kama ipo,kukubali situation uliyopo,kukubali kuna mambo huwezi kubadilisha na kuyaacha kama yalivyo.Sometimes kukubali kuwa PENZI ulilopo limefika kikomo usiforce upendo na mtu.Jua wakati wa kuwaacha watu waende na maisha yao na wewe uende na yako.Let people go...kulet go of the past,na zaidi kuwa strong kiimani....Amani ya moyo ni muhimu sana.Tujifunze kuutuliza moyo sio kuurusha rusha...Ukituliza moyo wako na akili yako itatulia.Bila amani ya moyo na utulivu wa akili hata ndoto zetu tutashindwa kuzifikia.
Good Morning!”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!