Wednesday 6 June 2018

Waishio na VVU waomba kusaidiwa ARV

Image result for dawa za ukimwi
Vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi (VVU) wameiomba serikali na wadau kwa ujumla kuwapatia dawa za kufubaza virusi (ARVs) ambazo matumizi yake ni angalau mara moja au mbili tu kwa mwezi.


Wamesema mbali na kuchoshwa na umezaji dawa kila siku, waathirika wengine, ambao wengi wao ni watoto hujisahau kumeza kwa kukosa uangalizi.
Inaelezwa kuwa wakati mwingine hukumbuka kumeza lakini si kwa wakati unaotakiwa, kitu ambacho ni hatari kwa maisha yao.
Wito huo umetolewa katika mkutano wa tano wa taifa wa watoto wanaoishi VVU uliokutanisha wadau mbali mbali kujadili mbinu zaidi za kuzuia maambukizi mapya kwa watoto.
Mwakilishi wa vijana kutoka Chama cha Watu Wanaoishi VVU Zanzibar (ZAPHA), Suhaila Msham mwenye umri wa miaka 19 amesema: "mbali na baadhi ya waathirika kutokuwa na waangalizi wa kuwakumbusha kumeza dawa, jamii yetu imejaa unyanyapaa. Ukimwi upo Zanzibar lakini jamii inachukulia kitu cha kawaida."
Alitolea mfano kwamba hata pale vijana wanapotembelea vituo vya afya kupima VVU kwa hiari, baadhi ya watoa huduma hukataa kwa kigezo kwamba ni lazima waambatane na wazazi wao. 
Sulahia ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Al-Haramain, aliomba serikali kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya VVU shuleni pamoja na kuhimiza matumizi ya ARVs kwa wale watakaobainika kuathirika.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!