Monday 26 March 2018

Lori laua watu 26 Pwani

WATU 26 wakiwemo watoto saba wamekufa jana usiku wakati lori lilipogongana na basi dogo la abiria kwenye Kijiji cha Kitonga, kata ya Mwalusembe wilayani Mkuranga, Pwani.


Kamanda wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Muslimu amesema ajali ilitokea saa tatu usiku ikihusisha magari mawili likiwemo lori aina ya Scania lenye namba za usajili T223 CZB lililokuwa na tela lenye namba za usajili T371 CBT, na Toyota Hiace yenye namba za sajili T676 DGK.
Lori hilo lilikuwa limebeba mifuko ya chumvi likitoka mkoani Lindi kwenda jijini Dares Salaam.
Basi dogo lilikuwa linatoka Mbagala kwenda Kimanzichana.
Watu wanane walijeruhiwa na wanapatiwa tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda Muslimu, dereva wa lori, bila tahadhari alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi katika eneo hilo ambalo kuna mteremko na kona hivyo gari likamshinda, likahama kutoka kushoto kwenda kulia na kugongana na basi dogo lililokuwa limebeba abiria.
Amesema katika ajali hiyo wamekufa wanawake 12, wanaume saba, na watoto saba wanaokisiwa kuwa na umri kuanzia mwaka mmoja hadi minne.
Dereva wa lori anapatiwa tiba chini ya ulinzi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!