Wednesday 7 March 2018

Fahamu juu ya Kansa ya Matiti (Ziwa)

Image result for kansa ya matiti
Kansa ya ziwa ni uvimbe wenye madhara (mkusanyiko wa seli za kansa) unaotokana na seli za ziwa. Pamoja na kuwa saratani ya ziwa huwaathiri zidi wanawake, huweza pia kuwapata wanaume. Kansa ya ziwa kwa wanaume hutokea kwa nadra, lakini pale itokeapo huleta madhara makubwa zaidi. 

Moja ya sababu ni kuchelewa kufanyiwa uchunguzi, inapotokea wanafanyiwa uchunguzi kansa hii huwa imefikia hatua ya kusambaa. Dalili za saratani ya ziwa kwa wanaume zinalingana na zule za wanawake, dalilil kuu ikiwa uvimbe ndani ya ziwa au kubadilika kwa rangi kulizunguka ziwa au kutoa majimaji. Kansa ya ziwa kwa wanaume huweza kutokea kwenye umri wo wote, lakini hujitokeza zaidi kwa wanaume wenye umri wa miaka 60 au zaidi. Katika mada yetu ya leo, tutazungumzia saratani ya ziwa ya wanawake.

Ziwa La Mwanamke
Ndani ya ziwa la mwanamke kuna sehemu kati ya 15 hadi 20 ziitwazo lobes. Kila moja ya sehemu hizi ina sehemu nyingi ndogo zaidi ziitwazo lobules. Lobules hizi zinz vikundi vya tezi ndogo zenye uwezo wa kutengeneza maziwa. Mtoto akizaliwa, maziwa hutiririka kutoka kwenye lobules kupitia mirija myembamba iitwayo ducts hadi kwenye chuchu. Mafuta na tishu za nyuzinyuzi hujaza nafasi kati ya lobules na mirija hiyo midogo.
Maziwa vile vile huwa na njia za limfu (lymph vessels). Njia hizi huelekea na kuungana na viungo vidogo vya mviringo viitwavyo lymph nodes. Vikundi vya lymph nodes vipo karibu na ziwa kwenye maeneo ya kwapa (axilla), juu ya mfupa wa mabega (collarbone), na kifuani nyuma ya breastbone.

Seli Za Kansa
Kansa huanza ndani ya seli, vitu vidogo vinavyojenga tishu. Tishu hujenga maziwa na sehemu nyingine za mwili.
Seli za kawaida hukua na kujigawa na kufanya seli nyingine kadri utakavyozihitaji. Seli za kawaida zikizeeka au kuharibika, hufa, na seli mpya huchukua nafasi yao.
Wakati mwingine utaratibu huu huenda kombo. Seli mpya huzaliwa wakati mwili hauhizitaji, na seli zilizozeeka au kuharibika hazifi kama inavyotakiwa. Kujijenga kwa seli hizi mpya hujenga uvimbe. Uvimbe katika ziwa unaweza kuwa hauna madhara au ukawa na madhara (kansa).
Uvimbe usio na madhara (benign tumors) unaweza kuondolewa na usirudie tena, hauvamii tishu za jirani na hausambai kwenye sehemu nyingine za mwili. Uvimbe wenye madhara (malignant tumors) unaweza kuondolewa lakini mara nyingi huota tena, huweza kuvamia na kuharibu tishu na viugo vya karibu, huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili.
Seli za saratani ya ziwa huweza kusambaa kwa kujitoa kutoka kwenye uvimbe wa awali. seli hizi huingia ndani ya njia za mfumo wa damu au mfumo wa limfu ambazo husambaa kwenye tishu zote za mwili. Seli hizi huweza kuonekana kwenye tezi za limfu karibu na ziwa. Seli hizi za kansa huwea kunasa kwenye tishu nyingine na kukua na kisha kujenga uvimbe utaoharibu tishu hizo. Kusambaa huko kwa seli za kansa huitwa metastasis.

Ni Zipi Aina Za Kansa Ya Maziwa?

Kuna aina nyingi za kansa ya ziwa. Kansa nyingine huonekana zaidi ya nyingine na kuna aina za kansa ambazo hutokea kwa pamoja. Aina za kansa ambazo hutokea mara nyingi Ni:
. Ductal carcinoma in situ:
. Invasive ductal carcinoma:
. Invasive lobular carcinoma:
.
.
. Mucinous carcinoma:
. Medullary carcinoma:
. Inflammatory breast cancer:
. Triple-negative breast cancers:
. Paget’s disease of the nipple:
. Lobular carcinoma in situ:
.
.
. Papillary carcima:
. Phyllodes tumor
. Angiosarcoma
. Tubular sarcoma

Hali Hatarishi Kwa Saratani Ya Ziwa Ni Zipi? Unapataje Kansa Ya Ziwa?


Ukiambiwa kuwa una saratani ya ziwa, kwanza utataka kujua ni nini hasa kilichosababisha saratani hiyo. Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayejua saratani hii inasababishwa na nini. Madaktari pia hawajui kwa nini mawanamke mmoja anapata saratani ya ziwa wakati mwingine hapati.
Lakini madaktari wanajua kuwa kuna mazingira au hali fulani vinachochea kutokea kwa kansa. Kuna hali zinazozuilika (kama unywaji wa pombe), na kuna hali ambazo haziwezi kuzuilika (kuzaliwa kwenye ukoo wenye historia ya saratani ya ziwa).
Utafiti umeonyesha mazingira na hali hatarishi kwa kansa ya ziwa kuwa ni:
. Umri:
. Historia binafsi ya afya:
. Historia ya afya ya familia:
. Mabadiliko ya jeni:
. Tiba ya mionzi kifuani:
. Historia ya uzazi na mzunguko wa hedhi:
. Jamii:
. Ujazo wa ziwa:
. Unene baada ya kukoma hedhi:
. Kukosa mazoezi ya mwili:
. Utumiaji wa pombe:

Dalili Za Saratani Ya Ziwa Ni zipi?



Saratani ya ziwa ya mwanzo kabisa kwa kawaida haitoi dalili zo zote. Kadri uvimbe utakavyokua, unaweza kubadlisha mwonekano wa ziwa au utofauti ukilitomasa. Mabadiliko yanayoonekana mara nyingi ni:
. Uvimbe au ngozi ngumu ndani au karibu na ziwa au maeneo ya chini ya kwapa
. Mabadiliko ya umbo au ukubwa wa ziwa
. Mikunyanzi juu ya ngozi ya ziwa
. Chuchu ya ziwa kurudi ndani
. Kutokwa majimaji kwenye chuchu na hasa yenye damu
. Magamba, wekundu au kuvimba kwa ngozi ya ziwa, chuchu au areola (eneo jeusi kwenye ngozi, katikati ya ziwa). Ngozi yaweza kuwa na matuta.
Yafaa kumwona mhudumu wa afya endapo mabadiliko yaliyotajwa yatadumu kwa muda mrefu. Baadhi ya dalili hizi si za kansa, tatizo jingine la afya laweza kuwa ndiyo chanzo. Hivyo basi, yafaa kufika kituo cha afya kwa uchunguzi wa kina zaidi na kupata tiba ipaswayo.
Hatua Za Kansa Ya Ziwa
Kama kipande cha tishu kimechukuliwa, kikapimwa na kuonekana kuwa na seli za kansa (biopsy), daktari wako atahitaji kujua hatua ya kansa iliyofikiwa ili ajue tiba unayostahili. Hatua ya kansa hutegemea ukubwa wa kansa, na kama kansa hiyo imeshashambulia tishu za jirani, na kama imeshasambaa kuelekea sehemu nyingine za mwili. Vipimo huchukuliwa kuja hatua iliyofikiwa na kansa hiyo.
Hatua za saratani ya ziwa ni:
Stage 0 mara nyingine inaamisha uwepo wa seli zisizo za kawaida ambazo si shambulizi. kwa mfano stage 0 huelezea ductal carcinoma in situ (DCIS). Mgonjwa huambiwa ana DCIS endapo seli zisizo za kawaida zitaonekana kutanda juu ya ngozi ya juu ya mirija ya maziwa (breast duct), lakini seli hizo hazijashambulia tishu za jirani za ziwa au kusambaa nje ya mirija. Ingawa madaktari wengi husema DCIS si kansa, wakati mwingine huweza kugeuka kansa ya ziwa kama tiba haikutolewa.
Stage I ni hatua ya awali ya mashambulizi ya kansa ya ziwa. Seli za kansa zimeshambulia tishu za ziwa nje ya eneo zilipoanzia, lakini seli hizo hazijatoka nje ya ziwa Uvimbe haujazidi kipimo cha upana wa sentimeta 2.
Stage II ni moja kati ya hali zifuatazo:
. Uvimbe hauzidi upana wa sentimeta 2. Kansa imesambaa hadi kwenye tezi za limfu zilizopo chini ya kwapa.
. Uvimbe ni kati ya sentimeta 2 na 5. Saratani haijafika kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa.
. Uvimbe ni kati ya sentimeta 2 na 5. Saratani imasambaa hadi kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa.
. Uvimbe ni zaidi ya sentimeta 5. Saratani haijafika kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa.

Stage III ni kansa ya sehemu moja iliyofikia hatua ya juu. hatua hii hugawanywa tena katika hatua za IIIA, IIIB na IIIC.
Stage IIIA moja ya hatua zifuatazo:
. Uvimbe haujazidi upana wa sentimeta 5. saratani imesambaa hadi kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa zilizoungana au zinazoungana na maungo mengine ya mwili. Au saratani imesambaahadi kwenye tezi za limfu zilizopo nyuma ya mfupa wa maziwa (breastbone).
. Uvimbe una upana wa zaidi ya sentimeta 5. Saratani imesambaa hadi kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa zilizo pekee au zilizoungana au kuungana na maungo mengine. au saratani imesambaa hadi kwenye tezi za limfu zilizopo nyuma ya mfupa wa ziwa.
Stage IIIB ni uvimbe wa ukubwa wo wote ule ulioota kwenye kuta za kifua au juu ya ngozi ya ziwa. Inaweza kuhusisha kuvimba kwa ziwa au uvimbe ndai ya ngozi ya ziwa:
. Uvimbe unaweza kuwa umesambaa hadi kwenye tezi za limfu za chini ya kwapa.
. Saratani inaweza kuwa imesambaa hadi kwenye rezi za limfu zilizopo chini ya kwapa zinazoungana au zinazoungana na maungo mengine. au, saratani imesambaa hadi kwenye tezi za limfu zilizo chini ya mfupa wa ziwa.
. Inflammatory breast cancer ni aina ya saratani inayoonekana mara chache sana. Ziwa huwa jekundu, lililovimba kwa sababu seli za kansa huziba mirija ya limfu kwenye ngozi ya ziwa. Dakatari agunduapo inflammatory breast cancer, huwa ni ya angalau hatua ya IIIB, lakini huweza kuwa ya hatua ya juu zaidi.
Stage IIIC ni uvimbe wa ukbwa wo wtw ule. Uvimbe huu umeshasambaa kwa moja ya njia zifuatazo:
. Uvimbe umesambaa hadi kwenye tezi za limfu nyuma ya mfupa wa ziwa na za chini ya kwapa.
. Saratani imesambaa hadi kwenye tezi za limfu juu ya au chini ya mfupa wa bega.
Stage IV ni kansa iliyosambaa maeneo ya mbali. kansa imesambaa kuelekea sehemu nyingine za mwili, kama mifupa, mapafu, au ubongo.

Ni Nini Tiba Ya Saratani Ya Ziwa?

Wanawake wenye saratani ya maziwa wana njia nyingi za kupata tiba. Tiba iliyofanya vizuri kwa mmoja si lazima ifanye kazi vizuri kwa mwingine. Tiba zinazotolewa ni upasuaji, mionzi, hormone therapy, chemotherapy na targeted therapy. Mgonjwa anaweza kupewa tiba za aina tofauti zaidi ya moja katika hizi.
Upasuaji na tiba za mionzi aina za tiba zinazotolewa kwenye ziwa lenyewe. Zinaondoa au kuharibu seli za kansa kwenye ziwa.
Hormone therapy, chemotherapy na targeted therapy hutumia dawa zinazoingia kwenye mfumo wa damu na kuua au kudhibiti saraatni mwili mzima.
Tiba ya kansa utakayopewa wewe mgonjwa itategemea vipimo vilivyochukuliwa, hatua ya kansa iliyofikiwa na afya yako kwa ujumla.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!