Saturday, 2 September 2017

Aina ya vyakula vinavyoweza kuhamasisha uzazi wako

Folic Acid
Kuna sababu kadhaa ambazo huweza kuchangia changamoto ya mwanamke kushika ujauzito, lakini leo naomba nikueleze mambo kadhaa ambayo yanaweza kukusaidia kushika ujauzito kwa haraka.




1. Kubadilisha mlo wako
Jitahidi kula vyakula muhimu vyenye virutubisho vinavyohitajika mwilini pamoja na madini mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na nazi, karanga, mayai, parachichi, mboga za majani, kabeji, maharage na broccoli.

Pia unaweza kula vyakula kama viazi vitamu na vingine vinavyofanana na hivyo ambavyo huongeza nguvu mwilini.

Wakati ukizingatia ulaji huo jitahidi pia kunywa maji ya kutosha na kuzingatia kupunguza ulaji wa vyakula vya viwandani.


2. Fanya mazoezi 
Mazoezi nayo ni muhimu kama unahitaji kushika ujauzito kirahisi, kwani mazoezi husaidia kuhamasisha homoni na hivyo kusogeza karibu uwezekano wa uzazi kwa akina mama na hata kinababa pia.

Unaweza kufanya mazoezi ya kutembea kila siku angalau kwa dakika 30 au hata kuogelea kwa muda fulani.

3. Jitahidi kuepuka msongo wa mawazo
Inafahamika kuwa ni vigumu kutokuwa na msongo wa mawazo hasa kwa wale wenye shida ya kutopata watoto, lakini unaweza kuamua kutosongwa na mawazo hayo na kuishi huru kwa muda fulani na huenda baadaye utajikuta ukishika ujauzito kwani inawezekana msongo wako wa mawazo unaweza kuwa chachu ya kuongeza ukubwa wa tatizo.

4. Acha kutumia/ vilevi/ sigara
Unapoamua kuwa mbali na bidhaa hizo unajiwekea uwezekano mkubwa wa kuweza kushika mimba kwani bidhaa hizo huweza kuchangia kuvuruga mfumo mzima wa homoni na hivyo kuchangia changamoto ya uzazi kwa mhusika.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!