Wednesday 30 August 2017

Watoto waliotekwa, wawili wapatikana Arusha

21192016_1516967388382516_842344448099418351_n.jpg
Siku moja mara baada ya Times Fm kuripoti habari kuhusu kupotea kwa watoto wanne, kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kupatikana kwa watoto wawili na kumshikilia mtu mmoja aliyekutwa na watoto katika kata ya olasiti .



Kamanda Mkumbo amesema jeshi la polisi linaendelea na upelelezi katika kuakikisha watekaji wote wanapatikana kwani tukio hilo sio la kufumbia macho na pia lina hatarisha amani kwa wakazi wa jiji la Arusha

wakizungumza na Habari Xtra wazazi waliowapata watoto wao kwa kuletewa na dereva wa boda boda mara baada ya watekaji kuwapatia namba ya balozi na kuagiza kuwarudisha nyumbani watoto wawili ,Ayub FRed na Bakari Suleman ,mama mzazi wa Bakari amesema ni faraja kuona mwanae amerudi salama nyumbani mara baada ya kumpoteza kwa siku nne mara baada ya kutekwa na watu wasio fahamika .

Amesema wazazi wengine wasikate tama kwani jeshi la polisi bado linaendelea na msako wa kuwapata watoto wengine wawili Maurin David pamoja na Ikram Salim ambapo mpaka sasa hawajulikani walipo .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!