Saturday 25 March 2017

Ukiwa MKWELI na MUWAZI hakuna lolote baya litakalokufika-Zamaradi Mketema


zamaradimketemaUkiwa MKWELI na MUWAZI hakuna lolote baya litakalokufika, lazima MUNGU akunusurishe na mabalaa..

 Simamia katika ukweli bila kumuonea wala kumtetea yoyote, unapokwazika na kuumizwa ongea, toa kinyongo, hakuna ubaya katika kuonesha maumivu kwa aliekukosea, maana mara nyingine unaemuwekea vinyongo huenda hata asijue na mzigo wa MAUMIVU ukawa unahangaika nao mwenyewe, usiwe mtu wa kunung'unikanung'unika pembeni na kulalama unajizibia Baraka tu na kukaribisha mabalaa, Kuongea kwa dhati KUNASAFISHA NAFSI na kukuacha huru. Atakaekutafsiri vibaya kwa ukweli wako hayo ni matatizo yake ila kama nia yako safi juu ya mtu ONGEA.. mwache Chuki aibebe yeye kama ataamua, asipokuelewa leo hata kesho ataelewa.#safishanafsi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!