Saturday 25 March 2017

Shilole: Nikichemka Muziki, Nakuwa Mama Lishe


STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameibuka na kusema kuwa endapo itatokea muziki ukambumia atageukia kazi ya mama ntilie ‘mama lishe’ kwa sababu anaipenda na iko kwenye damu.


Akibonga na Risasi Jumamosi, Shilole alisema tangu akiwa mdogo anapenda sana kupika hivyo hata sasa pamoja na kufanya muziki amekuwa akipika mwenyewe kwenye mgahawa wake aliofungua hivyo ikitokea kazi ya muziki imekataa atageukia kabisa kwenye kazi ya mama lishe kwani anaiweza na inalipa kuliko kawaida.
“Sioni aibu kuwa mama lishe maana ni kazi ninayoipenda na nikiacha muziki ndiyo itakuwa kazi yangu maalum sitahangaika na vitu vingine, sioni aibu kufanya kazi hiyo maana sina tabia za kuigiza maisha kama mastaa wengine, hapa penyewe huwa napika mwenyewe ili kuwafurahisha wateja wangu, namshukuru Mungu kazi hii inalipa kwani fedha ninazopata kwenye muziki huwa naziwekeza kwenye mtaji huu wa mama lishe,” alisema Shilole.
Chanzo:GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!