Monday 20 February 2017

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA MDAU AMSHUKURU MAKONDA


Kwanza kabisa napenda kumpongeza muheshimiwa P.Makonda..ni kijana mwenzetu anaonyesha moyo wa kutujali na kujali vijana..pili Tanzania imearibika juu ya hawa watu wanaodili na maafisa jeshi la polisi..mfano mwaka 2015 nilirudi Tanzania na gari aina ya BMW X4..naomba muheshimiwa unisikilize kwa makini.

Rommy akaipenda gari nimuuzie tukakubaliana nikampa gari nikabakia na karatasi za gari langu pindi atakapo nilipa nimpe document zote za gari.
Baada ya siku mbili akanipigia simu tukutane sinza makaburini.mie nikafika pale nikampigia mie nimeshafika lakini nilisikia back ground kuwa yuko na watu wanaongea ila sikutilia maanani.
Baada ya muda si mrefu akaja nikaingia kwenye gari lake akanipa fungu la dollar 9000 akachukua mfuko nyuma anipe pesa zingine za Tsh milioni18..wakati akiniwekea miguuni nikashitushwa na mlio wa bunduki na kio cha mlango wangu ambao ni wa abilia kimevunjwa na nikasikia tena milio mingi ya bunduki nikajump kutokea upande wa dereva na kukimbilia bite bite first food na watu waliokuwa pale first food walikimbilia wengine chooni.
Baada ya wale robers kuchukua pesa na kupanda pikipiki zao mie nikasaidiwa usafiri mpaka hospital ya palestina. Bwana rommy aliwaita watu wake alikuja Doto kutoka mabatini na swai kutoka osterbay nikakutana nao hospital na baadaye waliondoka na kuniambia niende kituoni baada ya matibabu.
Nilipofika kituoni nilimkuta rommy na Doto na polisi wengine wakiliongelea swala zima na kusema ya kuwa mie nimesharipwa pesa zangu na sina ninacho mdai..juu ya hapo wakachukua simu yangu baada ya rommy kuwaambia chukueni simu yake tukaichunguze kama siusiki na wale majambazi.
Nikamwambia Doto hivi nyie mnafanya kazi kwa hakili timamu au? Gari langu liko kwa Rommy mie niite watu waniibie pesa zangu kweli inawezekana...kama Gari lingekuwa kwangu na huu mchezo kutendeka basi mngehisi hivyo..na kama mnachukua simu yangu chukueni na yake.
Waka jifanya wamechukua na yake na yangu..baada ya mimi kuondoka pale kituoni gari zake Rommy akapewa na simu yake mie lofa awajanipa simu yangu muheshimiwa Paulo Makonda.
Kesho yake nikaenda central police nikatafuta jinsi ya kusaidiwa nikaelekezwa ofisi ya mtu niliye mtambua kwa jina la Ammy yeye ni mkubwa kwa cheo tena ni wa mkoa.nikamueleza hadithi yote..akasema huo ni mchezo wamekuchezea kwa kuwa hukai Dar unaishi Nje hivyo ngoja niongee na RCO WA OSTERBAY na ajawaambia na simu yangu nipewe.
RCO akasema niende kesho yake...na jioni ile nikarudi mabatini na kudai simu yangu..AFANDE DOTO alivyoniona akasema wewe ni mtoto wa mbunge..nikamwambia kwani mtoto wa mbunge peke yake ndio mwenye haki nipe simu niende kesho tutaonana kwa RCO.akanipa simu yangu nikaondoka.
Hivyo sikutendewa haki kwa sababu ya hizo pesa wabazopewa na hao watu.
Kesho yake nilienda kwa RCO nikampa habari yote! Akanyanyua simu akampigia Doto akamuuliza hizo gari zilizokuwa kwenye tukio ziko wapi akamjibu kachukua mwenyewe je mlipiga picha akajibu hapana akamwambia unakumbuka mkuu wa kituo cha magomeni alifukuzwa kazi kwa sababu kama hizi..naendelea kunukuu mheshimiwa akajibu ndio sasa nataka zile gari zirudi kituoni hapo na wewe na huyo Rommy nawaitaji sasa hivi hapa ofisini kwangu.
Kwakweli sikutendewa haki akamuru kwamba nilipwe pesa nusu katika zilizoubiwa yaani niliibiwa milion 18 kwa usemi wa Rummy sijazihesabu hivyo kwa kuwa nikuwa sina mtu wa kunisaidia na pale osterbay polisi wote wako upande wa Rummy wakaamuru tugawane ile hasara iliyopotea hivyo rummy atoe dollar 6000 tu kunilipa roho iliniuma lakini kwa kuwa sina uwezo badi haki yangu ya dollar 6000 ikapotea hivyo.
Nikabaki naomba mungu pia namshghulu sana afande Ammy kwa msaada wake kwani bila yeye mie na jella ningewekwa na kupewa kesi ambayo sijui lolote kwani nilisikia ndio ilikuwa wanifanyie hivyo ili wanile pesa..MUNGU AKULINDE MZEE (AFANDE ) AMMY NA PIA MUNGU AKULINDE MTENDA HAKI PAULO MAKONDA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!