Saturday 21 January 2017

Maamuzi mapya ya Rais Magufuli kwa Anne Kilango Malecela


Ni taarifa rasmi kutoka IKULU Dar es salaam juu ya maamuzi mapya ya Rais John Pombe Magufuli ambaye leo January 21 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge kwenye bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Cheo cha mwisho alichopewa Anne Kilango kilikua ni ukuu wa mkoa wa Shinyanga lakini April 11 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake na katibu tawala wa mkoa Abdul Rashid Dachi baada ya mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna Watumishi hewa.
Taarifa ya IKULU leo imesema baada ya Anne Kilango kuteuliwa, ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge.
KWA HISANI YA MILLARDAYO:COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!