Tuesday, 22 November 2016

Serikali yaahidi kumlinda kwa ghrama zote samaki aina ya papa Potwe.


Serikali wilayani Mafia mkoani Pwani imeahidi kushirikiana na wadau wa uhifadhi wa mazingira na maliasili za uvuvi wa bahari kumlinda kwa gharama zote samaki mkubwa kuliko wote duniani aina ya papa Potwe ambaye hapa nchini hapatikani mahali popote isipokuwa katika kisiwa cha Mafia wilayani humo.



Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani wilayani humo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Bw, Shaib Ahmed, katibu tawala wa wilaya hiyo Gilbert Sandagila amesema tangu kugunduliwa kwa samaki huyo amekuwa kivutio cha utalii ambapo amesema pamoja na vivutio vilivyopo serikali imejipanga kulinda samaki huyo na kumtumia kama sehemu ya utalii ili kuongeza pato la wilaya hiyo na uchumi wa taifa.
Kwa upande wake mratibu wa mradi shirikishi wa usimamizi wa rasilimali za bahari na uvuvi, kutoka shirika la uhifadhi wa mazingira na hazina ya wanyama duniani-WWF, Dkt. Mathias Igulu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujiepusha na uvuvi haramu kwakuwa vitendo hivyo vinaweza kusababisha kutoweka kwa papa Potwe na samaki wengine na hivyo kuathirika kiuchumi.
Baadhi ya wavuvi wa wilaya ya Mafia, wamesema wanamdhamini samaki huyo kwasababu amekuwa akirahisisha shughuli za uvuvi kwa vile anapotembea kutafuta chakula baharini huambatana na idadi kubwa ya samaki wadogo.
Maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani mwaka huu kwa wilaya ya mafia yalikuwa na kauli mbiu isemayo “tuwalinde papa Potwe,uhai wao ni faida kwetu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!