Wednesday, 25 May 2016

UPUNGUFU WA MAJI MWILINI KWA MTOTO MCHANGA(INFANT DEHYDRATION)

dlp4_061124030.ps

Upungufu wa  maji mwilini kwa watoto wachanga unaweza tokea wakati wowote.Upungufu wa maji unasababishwa na vitu tofauti kama joto kali ,mtoto kutonyonyeshwa baada ya muda mrefu  masaa 2-4, matatizo ya kiafya pia kuchangia mtoto kupoteza maji mwilini kama akitapika ,kuharisha au homa kali.


Kuna hatari kubwa kwa mtoto iwapo atapungukiwa maji mwilini .Mzazi atatambua vipi iwapi mtoto anaupungufu wa maji mwilini.

DALILI YA UPUNGUFU WA MAJI KWA MTOTO

:Mtoto kukojoa kwa mara chache sana inaweza chukua masaa 4-6 ,nepi au diaper inachukua muda kujaa na kuwa rangi ya njano na yenye harufu kali.

:Ngozi ukiivuta inachukua muda kurudi juu

:Mdomo na lips kuwa kavu sana mpaka kupasuka pasuka

:Hatokwi machozi akilia

:Kuishiwa nguvu na kupata tabu kupumua

:Kukosa hamu ya kula

:Macho ya mtoto yanalegea sana na kuingi ndani na

:Ngozi  kusinyaa kama ya mzee.

:Kwa mtoto mchanga utaona utosi wake unabonyea  ndani


soft-spot-on-newborn-babys-head
Utosi kubonyea kwa ndani ,bila kurudi juu.

Matatizo mengi  ya kiafya yanaweza jitokeza iwapo mtoto akapungukiwa maji  kwa muda mrefu, kama kupanda kwa joto kwa kiasi kikubwa ikapelekea kuadhiri  ubongo na organs nyingine mwilini,kusababisha kifo na matatizo mengine mengi ya kiafya.


 TIBA

Wahi kituo cha afya kwa msaada zaidi iwapo utaona hizo dalili.

Kwa mtoto mchanga ,mama unatakiwa mnyonyeshe mtoto kwa wingi kila baada ya dakika 30-60 na iwapo mnaishi kwenye mazingira yenye joto kali , unaweza mpa maji kidogo kijiko cha chai 2-3.

Watoto wenye umri zaidi ya mwaka 1 wanatakiwa kunywa maji kwa wingi zaidi na unaweza  kumtengenezea mchanganyiko wa maji ,chumvi na sukari akanywa.Usimveshe nguo nyingi au nguo nzito kwenye mazingira ya joto.

SHUKRANI KWA AFYA YA MTOTO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!