Monday, 23 May 2016

Neyo, Diamond watikisa Jembeka Festival


Mwanamuziki wa Marekani, Neyo (kulia) akiwa na

Mwanza. Wanamuziki, Diamond Platinum na NeYo walizikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza wakati wa tamasha la Jembeka Festival 2016 kwa nyimbo zao zilizobamba.


Katika tamasha hilo, wakali hao walipanda stejini kila mmoja kwa wakati wake na wadau waliofurika katika Uwanja wa CCM Kirumba lilipofanyika tamasha hilo walionekana kukubali kazi za wasanii hao.
Diamond ndiye alianza kupanda jukwaani na kuangusha ngoma zake zinazotamba kitaifa na kimataifa ikiwamo Onana, Make Me Sing, Utanipenda, Number One, Mdogomdogo, Nasema Nawe na Bum Bum.
Wakati anapanda ulingoni majira ya saa 12;35 mchana, wadau waliokuwa wamepooza walishindwa kuvumilia na kulipua shangwe huku wakisukumana kutaka kumuona ‘live’.
Ngoma iliyoonekana kuwakuna wadau wa burudani kwa staa huyo mshindi wa tuzo za MTV ni Make Me Sing na Bum Bum, ambazo alipoziimba aliitikiwa na umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo.
Burudani hiyo ilikolea baada ya Msanii NeYo alipopanda jukwaani kwa maringo na mapozi na kuwafanya wadau kuzua shangwe uwanjani hapo.
NeYo, msanii wa nchini Marekani alizikonga nyoyo za wana Mwanza alipoanza kuimba wimbo wa Miss Independent, Because of You, ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwafanya wapenzi wa burudani kuanza kucheza.
Wasanii wengine waliotikisa jukwaani hapo ni Juma Nature, Fid Q, Rubby, Nay wa Mitego, Mo Music, Mr.Blue, Baraka Da Prince.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!