Thursday, 26 May 2016

MO DEWJI ATAJWA KUWA MWAJIRI MKUBWA AFRIKA




Mohammed Dewji
Dar es Salaam. Mohammed Dewji ametajwa tena kwenye orodha ya mabilionea wa Afrika ambao ni waajiri wakubwa.

Mwanzo alitajwa kuwa ni mmoja wa mabilionea na baadaye akashinda kuwa tajiri kijana zaidi mwenye miaka chini ya 40. Mtandao wa Face2Face Africa umetoa orodha ya matajiri watano wanaotengeneza fedha nyingi kutoka Afrika na kuajiri Waafrika wengi. Kwenye orodha hiyo mpya, Dewji ameshika nafasi ya tano akiwa na wafanyakazi 24,000, kwa mujibu wa mtandao huo. Lakini mwenyewe anasema idadi hiyo imekosewa.“Kuna zaidi ya watu 28,000 wanaofanya kazi kwenye kampuni yangu,” alisema.
Mpaka Machi mwaka huu, takwimu zinaonyesha kulikuwa na mabilionea 24.
Dewji ameingia kwenye orodha hiyo kutokana na kuwekeza utajiri wake wa Dola za Marekani 1.25 bilioni (zaidi ya Sh2.5 trilioni).
Fedha hizo zimewekezwa na Mohammed Enterprises Limited Group (Metl) kwenye usafirishaji, kilimo na uzalishaji.
Aliko Dangote bilionea wa Nigeria ndiye anayeongoza orodha hiyo kwa utajiri wake wa Dola 25 bilioni (zaidi ya Sh50 trilioni) ambaye kampuni yake ya Dangote Group imewekeza katika nchi 16 Afrika.
Anayefuatia kwa Dangote ni Christo Wiese, mmiliki wa Shoprite yenye matawi zaidi ya 2,800 duniani. Wiese ameajiri wafanyakazi zaidi ya 160,000. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Naguib Onsi Sawiris kutoka Misri. Mwenyekiti huyo wa kampuni ya Orascom ana utajiri wa Dola 3.1 bilioni, lakini anatajwa kuajiri Waafrika wengi zaidi.
Pamoja na Dewji aliyeachia ubunge wa Jimbo la Singida Mjini mwaka jana, yumo pia Issad Rehab, bilionea wa Algeria ambaye ukwasi wake unakadiriwa kufikia Dola 3.5 bilioni.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!