Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akipita mbele ya jeneza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (kulia) akimpa pole mke wa Marehemu Kabwe aitwaye Faith Kabwe.
Viongozi mbalimbali wakipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.
Mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) akipita mbele ya jeneza.
Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
Mamia ya waombolezaji wakiwa katika mstari kutoa heshima zao
Walioko mbele ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Waziri George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee Dar.
Mke wa marehemu Kabwe, Faith Kabwe (wa kwanza kulia) akiongozana na wanafamilia walipofika viwanja vya Karimjee.
Jeneza lenye mwili likiwa limebebwa na waombolezaji.
Kamanda Maalumwa wa Mkoa wa Kipolisi jijini Dar, Simon Sirro (kushoto) akiwa viwanjani hapo.
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakiwemo viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, walijitokeza kwenye viwanja vya Karimjee, Dar, kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mbonea Wilson Kabwe.
Akizungumza katika maombolezo hayo, waziri Simbachawene aliwapa pole wafiwa kwa msiba huo na kutoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Magufuli.
”Tumepata pigo kama serikali, hakika atakumbukwa kwa mema na mchango alioutoa enzi za uhai wake, nitaungana na wafiwa kuelekea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumpumzisha mpendwa wetu,” alisema Simbachawene.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliungana na ndugu jamaa na marafika katika maombolezo hayo huku akisema kuwa kwa niaba ya mkoa wa Dar es Salaam anatoa pole kwa wafiwa.
Mwili wa marehemu, Wilson Kabwe umesafirishwa kuelekea kijijini Mamba Wilayani Same kwa ajili ya mazishi.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment