Tuesday, 24 May 2016

Kesi ya ‘Malkia wa Pembe’ yaahirishwa tena Tanzania

YangImage copyrightAFP
Image captionYang alifika Tanzania kwa mara ya kwanza miaka ya 1970
Kesi dhidi ya mwanamke Mchina ambaye anatuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa pembe za ndovu kutoka Tanzania imeahirishwa tena.


Kesi hiyo dhidi ya Yang Fenglan, maarufu kama ‘Malkia wa Pembe’ imeahirishwa hadi tarehe 6 Juni.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama kwamba faili ya kesi hiyo bado imo mikononi mwa afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.
Maafisa hao wameambia mahakama kwamba wanatarajia kuipata faili hiyo kabla ya tarehe 6 mwezi Juni.
Kesi hiyo ilikuwa awali imetarajiwa kuanza Dar es Salaam tarehe 9 Mei lakini ikaahirishwa kwa wiki mbili.
Yang, 66, anatuhumiwa kuongoza kundi la walanguzi waliohusika kusafirisha pembe karibu 700 za ndovu za thamani ya $2.5m (£1.7m) kutoka Tanzania hadi mataifa ya Mashariki ya Mbali.
BBC

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!