Challenge kubwa tuliyonayo ni kukua kwetu kiakili,kihisia na kiimani.Na vyote hivi haviwezi kuja kama hujapitia changamoto za kimaisha.Changamoto ndio hutufanya tukomae kiakili,kimawazo,kihisia na kiimani.
Inahitaji uthubutu kusimama tena kama ulianguka na kuanza upya.Na yote yakawezekana kama una Imani ndani yako.Wewe angalia ni maeneo gani umeanguka na kuwa defeated.Imani hukupa sababu ya kuumba kile unachotaka kiwe,kile unachoamini kinakufaa kitokee na kinatokea ukiamini..ukomavu wa kiimani na zaidi kama Mungu umemshirikisha.
Katikati ya changamoto ndipo unajifunza ku control hisia zako za hasira na maumivu.Hutaki kupelekeshwa na hasira au maumivu japo ni ruksa kuumia na kuomboleza.Kama hauta mudu kupambana na hisia hizi zitakuumiza na kukufanya ushindwe kusonga or ukawa kichekesho.Ukiweza hili eneo hapa ndio kuna ukomavu wa kihisia,kuachilia nakusamehe kama inabidi.
Usiogope,Uoga kila mtu anao na tunayoyaogopa sio ya kweli ila yapo mawazoni mwetu.Uoga huua ndoto,huua matumaini,Uoga unaweza kukufanya uumwe,uoga unaweza kukufanya urudi nyuma na usifanye jambo ambalo ndani yako unajua umekuwa ukilitamani kwa muda mrefu na uwezo wa kulifanya unao.Uoga unakufanya uparalyze kabisa usiweze kujisogeza.
Lakini kuogopa pia ni kuchagua ....wakati ukiogopa ndani yako unajua kabisa kuna mtu unataka kuwa,kuna mahali unataka kuwa,unajua ulipo sio mahali sahihi lakini umechagua kuogopa.
Lakini ukiacha kuogopa utazipigania ndoto zako,utaipigania amani ya moyo wako,utaipigania afya yako,utakamata usukani wa maisha yako na kujipeleka unapopaswa kuwa.
Kubali ulipo kwa sasa yes lakini beba ipasavyo jukumu la kujipeleka kule unapotaka kwenda kamata usukani sawa sawa na kuwa dereva wa maisha yako.
DINA MARIOS!
DINA MARIOS!
No comments:
Post a Comment