
Kutoka Ikulu Dar es salaam leo March 6 2016, ni uteuzi mpya uliofanywa na Rais John Pombe Magufuli kwa kumteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu kiongozi ambapo kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.
Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amesema aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Rais Magufuli
March 6 2016 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuliamemtangaza katibu mkuu kiongozi mpya kwenye serikali yake ambaye anachukua nafasi hiyo iliyokua kwa Ombeni Sefue, katibu mkuu mpya amekua akifanya kazi kama Balozi wa Tanzania India, mtazame Rais Magufuli hapa chini.













No comments:
Post a Comment