Wednesday, 9 March 2016

Marufuku sukari kuuzwa zaidi ya Sh2,000 D’ Salaam

“Hakuna haja ya kuagiza sukari kutoka nje kwa

Dar es Salaam. Serikali imetangaza bei elekezi ya Sukari kwa Mkoa wa Dar es Salaam na ile ya jirani kuwa iuzwe Sh2,000 kwa kilo moja.



Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwaza alisema jana kuwa wafanyabiashara watakaokiuka amri hiyo kwa kuuza sukari kuvuka bei hiyo watachukuliwa hatua.
Alisema katika mikoa ya mbali na Dar es Salaam inayohitaji gharama kubwa za usafirishaji ukiwamo wa Kigoma, bidhaa hiyo itauzwa kwa Sh2, 200.

Semwaza alisema wafanyabiashara hawatakiwi kuzidisha bei na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wa halmashauri husika kwa atakayekiuka agizo hilo elekezi. “Nilifanya kikao na wafanyabiashara, nimegundua wanaficha sukari ili iadimike na wao waje kuuza kwa bei wanayotaka, kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Sukari Kifungu cha 26 ya mwaka 2001 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2009, kuficha sukari ni kinyume na sheria na atakayekiuka amri ya Serikali atachukuliwa hatua za kisheria,” alisema.
Alisema hatua ya kuweka bei elekezi imekuja ili kukabiliana na wafanyabiashara wanaopandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela.
Alisema Kampuni ya Alneem Enterprise ina tani 8,600 za sukari na wameiagiza iiuze kwenye maghala ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
“Hivyo kama Bodi ya Sukari tukishirikiana na Kamati ya Ufundi ya Uagizaji sukari na Sekretarieti za mikoa, tunasisitiza tutaendelea kufuatilia kwa karibu kiasi cha sukari kilichopo nchini na mwenendo wa bei na kuchukua hatua dhidi ya watakaoharibu mwenendo wa soko na kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa soko,” alisema Semwaza.
Alisema pia wamekitaka Kiwanda cha Sukari cha TPC kuuza sukari yote iliyopo na inayoendelea kuzalishwa badala ya kuuza kidogo kidogo na kusababisha taharuki katika soko la bidhaa hiyo.
Pia, alisema wameagiza kiwanda cha sukari Kilombero kuwataka wafanyabiashara waliolipia sukari waliyozalisha kuingiza sokoni badala ya kuendelea kuihifadhi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!