
Ajali mbaya imetokea mapema leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi- Dar es Salaam ikihusisha magari matatu, daladala (DCM) iliyokuwa na abiria lifanyalo safari zake Gongo la Mboto na Simu2000, Lori lililobeba mchanga na Lori lililokuwa limebeba N’gombe likielekea Vingunguti
Watu ambao idadi yao bado haijafahamika maramoja wanasadikiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali hiyo.




Maofisa wa Polisi wakiwa eneo la tukio.


KWA MUJIBU WA SHAHIDI ALIYESHUHUDIA AJALI HIYO:
Mwenye ndugu jamaa au rafiki anaekaa Gongo La Mboto na anafanya kazi ubungo au alikuwa akielekea ubungo alfajiri ya leo... amtafute huyo ndugu jamaa au rafiki yake kujua kama ni mzima au laa...
maana kuna ajali imetokea matumbi ikihusisha daladala(DCM) la G/Mboto-Ubungo na Lori la Mizigo pamoja na Lori lililokuwa limebeba ng’ombe
kweny DCM waliopona ni watu wasiofika watano... yale malori mengine hajatoka mtu hata mmoja... mbaya ni kwamba DCM lilikuwa limejaza abiria mpaka wengine wakasimama
Ajari ni mbaya sana mpaka nimeshindwa kupiga picha maana DCM lilivyofanywa si rahisi kulitazama kwa mda mrefu😰
Ajali imetokea pale kabla hujafika Tabata Matumbi Pale Darajani
R.I.P Wote Waliofariki













No comments:
Post a Comment