Tuesday 9 February 2016

MKE WA MIZENGO PINDA ANUSURIKA AJALINI MOROGORO



Mke wa waziri mkuu wa zamani, Tunu Pinda     

Mke wa waziri mkuu wa zamani, Tunu Pinda jana alipata ajali wakati akitokea mkoani Dodoma baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka na kumgonga mwendesha pikipiki aliyefariki eneo la tukio.



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutegwe aliwaambia waandishi wa habari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kuwa gari hilo aina ya Toyota Landcruser ambalo ni mali ya Serikali, lilikuwa likimkwepa mwendesha pikipiki alikuwa akiingia barabara kuu bila kuangalia.
Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Lita Lyamuya alisema hali za wagonjwa kwa sasa zinaendelea vizuri na tayari wameruhusiwa kuendelea na safari yao ya Dar es Salaam.
Dk Lyamuya alisema alipokea majeruhi wanne ambao ni Mama Tunu Pinda, mlinzi wake Gaudensia Tembo(40), Angelo Mwisa (50) ambaye ni dereva wa gari hilo na Girbert Sampa(40) ambaye ni ndugu na Mama Pinda.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Michael Salumu alisema alisikia kishindo akiwa ndani ya nyumba yake na alipotoka nje, alikuta gari hilo likiwa limepinduka na kuona wanawake wawili na mwanaume mmoja wakiwa wameumia sehemu za uso na mbele yake kukiwa na pikipiki.

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!