Thursday, 7 January 2016

WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI YA MTO-KIGOMA

WATU wanne wamefariki dunia baada ya kuosombwa na maji ya mto nkonko uliopo katika Vijiji vya Nyalubanda na Mkigo Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma kutokana na mto huo kujaa maji baada ya kunyesha mvua kubwa. 

Akizungumza na blog hili kuhusu tukio hilo, Mtendaji wa kijiji cha Nyarubanda, Narberth Mchemwa alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Januari 5 baada ya mvua kubwa kunyesha kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa 11 hivyo kusababisha mto huo kujaa maji.

Alisema kuwa, watu hao walisombwa na mto huo wakati wakijaribu kuvuka ambapo kutokana na wingi wa maji watu hao walisombwa na kusababisha vifo vyao. 

Aidha Mchemwa alisema kuwa, mpaka sasa maiti zilizoonekana ni miili minne na wanaendelea na uchunguzi ilikupata miili mingine.

"Waliofariki ni Kezia Leonard(35), Melisia Moshi (18), Julio Jonasi (13) na mwingine jina lake halijafahamika "alisema Mchemwa. 

Hata hivyo Mchemwa alisema kuwa, miili ya marehemu itafanyiwa mazishi leo hii ila bado polisi wanaendelea kutafta miili mengine kutokana na baadhi ya wakazi wa Vijiji hivyo kudai kuwapoteza ndugu zao bila kufahamu walipoelekea.

Nae Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na Aliongeza Kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ilikubaini miili mingine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!