Wednesday 6 January 2016

CHAKULA CHA LEO! MASHED POTATO WITH CHICKEN!



Mashed potato with chicken ni chakula kizuri sana na radha nzuri, chakula hiki waweza kula wakati wowote na kinywaji chochote. Pia chakula hiki anaweza kula mtoto mdogo.
Kuandaa: dakika 10 
Mapishi: dakika 30

Mahitaji


  • Kuku aliyetolewa ngozi tayari robo kilo
  • Butter vijiko 2
  • Pilipili manga kijiko 1 chai
  • Nyanya 2
  • Nyanya ya kopo kijiko 1
  • Tangawizi iliyosagwa kijiko 1
  • Viazi ulaya robo kilo
  • Chumvi kijiko kimoja cha chai
  • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
  • Kitunguu maji 1
  • karoti 1
  • Pilipili hoho 1
  • Gram masala kijiko 1

Maelekezo

  • Chemsha kuku, weka tangawizi, kitunguu saumu, mkamulie ndimu na chumvi. Hakikisha ameiva na supu imebaki kidogo.
  • Toa nyama iweke kwenye chombo pembeni, tayari kwa kuliwa.
  • Chukua sufuria, weka butter kijiko kimoja ikipata moto weka kitunguu maji, kitunguu saumu, pilipilipili hoho na karoti, koroga mboga ziive ila zisiive sana.
  • Weka nyanya ikichemka, weka nyanya ya kopo na gram masala koroga mpaka uhakikishe nyanya vimeiva kisha ongeza maji kidogo, funika sauce ichemke kisha epua weka pembeni.
  • Menya viazi, kata saizi unayotaka, weka supu ya kuku kidogo, hakikisha viazi vinaiva na havipondeki.
  • Vikiiva epua, weka viazi kwenye bakuli au sufuria, weka pilipili manga, butter yenye chumvi na maziwa kwenye viazi.
  • Anza kuponda viazi, viponde kwa mwiko au visage kwenye blender hakikisha visiwe uji, viwe kama ugali.
  • Ukiona tayari weka pembeni.
  • Chukua sahani pakua viazi, weka sauce na kipande cha kuku, hapo utakua tayari kujiramba.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!