Wednesday 6 January 2016

BOMOA BOMOA YAKUMBA NYUMBA 100 MANISPAA YA KINONDONI


BOMOABOMOA katika Manispaa ya Kinondoni imeendelea jana kwa nyumba takribani 100 kubomolewa kwa watu waishio mabondeni huku waliotakiwa kuhama katika hifadhi za misitu ya mikoko kufanya hivyo ifikapo kesho.


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Bonaventure Baya alisema ubomoaji huo ulioanza jana baada ya kusitishwa wakati wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya. Nyumba zipatazo 100 zilibomolewa jana katika eneo la Jangwani.
“Ubomoaji umeanza leo (jana) asubuhi kama kawaida na hadi mchana huu nyumba takribani 100 zimeshabomolewa katika eneo hilo la Jangwani, na kazi inaendelea vyema,” alisema Baya.
Akizungumzia bomoabomoa hiyo, Baya alisema ilikuwa ya amani na utulivu mkubwa kwani katika nyumba hizo zote walizokwisha kubomoa na nyingine zaidi ya 200 katika eneo hilo zipo wazi kwa maana wenye nazo wameshahama, jambo ambalo limerahisisha kazi hiyo.
Hata hivyo, wakati shughuli hiyo ikiendelea, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, jana imeitaka serikali kusitisha kwa muda ubomoaji wa nyumba za watu 681 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Jaji Panterine Kente alitoa amri hiyo baada ya kupitia hoja za pande zote katika maombi ya uwakilishi wa kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye maeneo oevu na ya wazi katika manispaa hiyo.
Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Kente aliitaka serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kusitisha kwa muda zoezi la ubomoaji wa nyumba za waleta maombi hadi shauri lao litakapofunguliwa, kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
Alisema ili kurahisisha utekelezaji wa amri hiyo, mawakili wa upande wa waombaji waliwasilisha mahakamani, orodha ya majina na anuani pamoja na maeneo zilipo nyumba za waombaji wote.
Aidha alisema serikali haizuiwi kuendelea na zoezi la kupima, kuweka alama na kama ikibidi kubomoa nyumba za wakazi ambao siyo wahusika katika shauri lililopo mahakamani.
Maombi hayo yamewasilishwa na wakazi 681 wa kata tatu za Kinondoni, kupitia kwa mawakili wao Abubakari Salim pamoja na George Mwalali, wakiomba kuwakilishwa na wenzao saba, ili wafungue kesi dhidi ya AG, Manispaa ya Kinondoni na NEMC.
Akisoma uamuzi huo jana, Jaji Kente alisema kabla ya kusikilizwa kwa maombi hayo, waleta maombi waliiomba Mahakama itoe amri ya kusitisha kwa muda zoezi la ubomoaji wa nyumba zao wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo.
Hata hivyo upande wa wajibu maombi uliowakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na Burton Mahenge ulipinga kwa madai katika hatua ya shauri hilo, Mahakama haina mamlaka ya kutoa amri yoyote kwa kuwa ni maombi ya kufungua kesi hivyo hakuna shauri lililopo mahakamani.
Aidha Malata alidai waleta maombi hawajawasilisha orodha ya majina yao hivyo Mahakama ikitoa amri itafanya hivyo kwa watu ambao haiwafahamu. Katika uamuzi wake Jaji Kente alisema, anakubaliana na hoja ya Malata lakini kwa mujibu wa Mwenendo wa Mashauri ya Madai, kesi inakuwa imefunguliwa endapo wahusika watawasilisha maombi mahakamani, pia katika uamuzi wa Mahakama ya India, hata kama kesi haijafunguliwa, Mahakama inaweza kutoa amri endapo itaona kuna haja ya kufanya hivyo.
Wakazi hao waliokuwa wamekaa nje ya Mahakama, baada ya kuambiwa uamuzi huo na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia, walianza kufurahi na kupiga kelele jambo lililosababisha askari wengi kufika katika eneo hilo wakiwa na gari la maji ya kuwasha.
Hata hivyo walitawanyika kwa amani. Wakati huo huo watu wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu ya mikoko, kesho ndiyo muda wa ukomo wa agizo la kutakiwa kuhama. Wadau

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!