Friday 4 September 2015

EBOLA YATATIZA TENA SIERRA LEONE

Maafisa wa kukabili EbolaImage copyright
Image captionMaafisa wa kukabiliana na Ebola
Watu 1,000 nchini Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki kutokana na Ebola.
Hilo limejiri siku tano tu baada ya kuanza kwa hesabu ya wiki sita iliyolenga kutangaza taifa hilo kuwa bila Ebola.


Karantini hiyo itadumu wiki tatu, mradi tu kusiwe na visa vipya vitakavyoripotiwa.
Watu Zaidi ya 11,000 wamefariki tangu kuanza kwa mkurupuko wa Ebola nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia.
Mwandishi wa BBC Umaru Fofana katika mji mkuu wa Freetown, anasema maafisa wa serikali nchini humo walikuwa na matumaini baada ya kupita kwa kipindi kirefu bila kisa kipya cha Ebola na kwamba kisa cha sasa kimewashangaza.
Mwandishi wetu anasema karantini ya sasa ina masharti makali zaidi kuliko za awali. Ni pamoja na amri ya kuzuia watu kutembea kutoka nyumba moja hadi nyingine.
Wanajeshi na maafisa wa polisi wametumwa kudumisha karantini hiyo katika kijiji cha Sellakaffta, kilichoko Kambia kwenye mpaka wa kaskazini wa taifa hilo na Guinea.
Maafisa wa Shirika la Afya Duniani na wizara ya afya Sierra Leone wanapanga kutoa chanjo kwa wale ambao huenda walikutana na mwanamke huyo.
Guinea inajaribu kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa huo nchini humo. Liberia, WHO ilitangaza kuwa virusi vya Ebola vimeacha kusambaa kwa mara ya pili Alhamisi.
Taifa hilo lilitangazwa kutokuwa na Ebola mwezi Mei lakini visa zaidi vikaripotiwa mwezi uliofuata.
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!