Thursday, 13 August 2015

VIJANA CHAGUENI VIONGOZI WENYE MANUFAA KWA TAIFA

WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imehimiza vijana kuhakikisha wanachagua viongozi wenye maslahi kwa taifa katika uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel alitoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.


Aliwataka vijana watumie haki yao ya msingi, kupiga kura na kuchagua wanaowahitaji na ambao wataleta maendeleo nchini. “Chagueni viongozi wenye maslahi kwa taifa kwani kura zenu ndio zenye kuonesha mnahitaji Tanzania ya aina gani,” alisema Profesa Gabriel.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem alisema kwa Tanzania wapo vijana milioni 1.8 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Aliwataka vijana kutumia wingi wao kuwa imara na kuwa sehemu ya uamuzi, kushiriki katika ngazi za maendeleo, kutambua ndoto zao na kuzitumia ipasavyo katika kukuza uchumi.
“Ushiriki wa vijana ni suala la haki za binadamu… asilimia 90 ya vijana wanaishi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo waamke na kuwa chachu ya maendeleo,” alisema Dk. Kenan. Akisoma mapendekezo ya vijana, Hussein Melele alisema ni wakati sasa kwa serikali kuhakikisha inawashirikisha kwenye nyanja mbalimbali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!