Thursday, 13 August 2015

JK AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM MJINI DODOMA KINACHOPITIA MAJINA YA WALIOPENDEKEZWA KWENYE NAFASI ZA UBUNGE

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo majina mbali mbali yaliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge yalipitiwa,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phiip Mangula, na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ambacho kinapitia majina ya yaliopendekezwa kwenye nafasi za ubunge.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipitia majina ya waliopendekezwa kwenye nafasi za Ubunge.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ,Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma kujadili majina ya waliopendekezwa kwa nafasi za Ubunge kupitia CCM, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa kwenye mazungumza kabla ya kuanza kwa kikao kutoka kushoto ni Dk. Salim Ahmed Salim, Mama Salma Kikwete na Shamsi Vuai Nahodha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Dk.Salim Ahmed Salim kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na Dk.Salim Ahmed Salim kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Spika la Bunge la Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda akizungumza na Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Khamis Juma kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu mjini Dodoma.
Wajumbe wa NEC wakizungumza kabla ya kuanza kwa kikao, kutoka kushoto ni Ridhwan Kikwete, Mohamed Nyundo na Anthony Mavunde.
 Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mama Zakhia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kiakoa cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mama Zakhia Meghji akizungumza na Katibu Mkuu wa UWT Amina Mwakilagi kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini yanayoendelea kwenye kikao cha NEC, kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Ndugu Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Zaidi ya wajumbe 366 walihudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa
Tanzania Ndugu Mizengo Pinda wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!