Wednesday, 12 August 2015

ULIYAJUA? MATUMIZI YA KARANGA KWA UJI WA MTOTO

image

Matumizi ya karanga kwa uji wa mtoto ni vizuri sababu inamwongezea virutubisho ,mafuta na kumsaidia kulainisha choo ila karanga haitakiwi kukaa kwa mda mrefu baada ya kusagwa.


Karanga inatabia ya kutengeneza fangasi hivyo utakapo andaa nafaka(mfano -ulezi,mahindi,mchele,ngano….) za kutengeneza unga wa lishe haipaswi kuchanga’nya na karanga ,iwapo utasaga nafaka usichanganye na karanga,karanga saga pembeni na isiwe nyingi saga ya kutosha itakayo tumika wiki moja (siku 7) na unatakiwa uhifadhi sehemu kavu  na safi kwenye chombo cha plastik chenye mfuniko.


image

Utakapo pika uji baada ya dakika 10 ongezea karanga vijiko 2-3 vikubwa ,koroga na acha karanga iive vizuri ndio uepue tayari kumpa mtoto,uji wa lishe unatakiwa kupikwa kwa mda mrefu sichini ya dakika 35-45 moto usiwe mkali ,sababu huo mchanganyiko wa nafaka  na karanga uive vizuri lasivyo mtoto ataharisha.

JINSI YA KUANDAA KARANGA


Chambua karanga vizuri ondoa zile mbovu na pepeta kwenye ungo,andaa moto usiwe mkali mdogo tu, bandika sufuria na kukaanga bila mafuta zikibadili rangi kidogo  epua. Anika juani zikikauka toa maganda yake na kuchambua tena kutoa zilizoungua au mbovu ,tayari kusagwa kwa blender au kutwanga na kinu au peleka mashine ila hakikisha unafanya kwa hali ya usafi. Baada ya kusagwa hifadhi kwenye chombo cha plastik na kufunika hakikisha isikae zaidi ya siku 7.

image

MADHARA YA KUCHANG’ANYA KARANGA NA NAFAKA ZA(UNGA WA LISHE) WAKATI WA KUSAGA!

Karanga inatabia ya kuotesha fungus na  kutengenza sumu ya toxin inakuja kuadhiri ini la mtoto na kumpelekea kupata saratani ya ini daktari bingwa wa watoto hospital ya muhimbili Dr Masawe anashauri karanga iandaliwe kidogo na itumike wakati wa kupika uji , karanga inatabia ya kuungua / kunata kwenye sufuria mapema kabla uji haujaiva, hapo unakuwa  unapoteza vitutubisho vyote vilivyomo hivyo ni vizuri ukafatilia maelezo nilio toa hapo juu jinsi ya kutumia karanga kwa njia sahihi.




Ushauri wa afyaborakwamtoto


Unaponunua / tengeneza   unga wa lishe usinunue / kutengeneza wenye mchanganyiko wa

 image

1:Nafaka zaidi ya mbili yani kama ni (mahindi,soya,uwele,mtama na nyinginezo) badala yake nunua wenye nafaka 1-2 tu ,kwani mchang’ayiko mkubwa sio mzuri kwa mtoto unahatarisha afya yake sababu utumbo(mfumo wa mmeng’nyo) wake hauna uwezo wa kumeng’enya vyote hivyo kwa wakati 1bado ni mdogo na utamfunga choo


2:Usinunue unga wa lishe wenye soya ndani kwa watoto chini ya miaka 2


3:Usinunue uji wa lishe wenye mchanganyiko wa karanga

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!