Wednesday, 12 August 2015

ERIC SAMUEL NA NENO JUU YA WANAWAKE!


HESHIMA KWA MWANAMKE
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKEWA WANAUME
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape,heshima zao wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!