Saturday, 4 July 2015
TATIZO WASOMI MNATUMIA AKILI NYINGI KWENYE JAMBO DOGO. Ona hii!
Msomi mmoja mwenye PhD
pamoja na
kijana mmoja ambaye hakubahatika
kusoma walisafiri pamoja
kwenda
kutembelea mbuga moja
maarufu yenye
maua na ndege wa kuvutia. Usiku ulipofika wakaweka hema
lao
zuri na la kisasa na wakalala
usingizi
mzito kabisa.
Masaa machache baadae, Yule kijana
asiye msomi akamuamsha yule
msomi
na kumwambia 'hebu angalia
angani
kisha niambie umegundua nini?' Jamaa mwenye PhD aka jibu:
"Naona
mamilioni ya nyota na
mbalamwezi.'
Yule kijana asiye msomi akauliza
tena “Unajifunza nini ukiona hivyo?”
Msomi akatafakari kwa dakika
kadhaa
kisha akajibu: "Upande wa
kiunajimu
inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi
sana katika hii dunia kwetu
wanadamu..... Upande wa muda
inaonyesha ni usiku wa
manane....
Upande wa imani inadhihirisha kuwa
Mungu ni muweza wa vyote na
sisi
kwake ni viumbe wadogo sana
na tusio
na mamlaka... Upande wa hali ya hewa.... kesho itakuwa siku nzuri
sana".
PhD kisha naye akauliza.... kwa
upande
wako wewe umegundua nini?”
Yule jamaa asiye msomi akakaa kimya
kwa muda na kisha akajibu:
“Kiuhalisia.... mimi nimegundua
kuwa …
Hema letu limeibiwa!!Haha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment