Wednesday, 8 July 2015
CHANZO CHA KIUNGULIA WAKATI WA FUNGA:
Ulaji usio sahihi mfano kula futari zinazochelewa kusagika na kuyeyuka tumboni kama mchele,ngano,maharagwe nk yenye mafuta/chumvi/sukari nyingi na unywaji wa maji,juisi,soda nk wakati wa kufungua ndio chimbuko la kiungulia'flatuence/heartburn'hali ambayo ikiendelea kuwepo zaidi ya mara mbili kwa wiki hugeuka kuwa ugonjwa tuliokwishaona'GERD-Gastroesophageal Reflux Disease'.
DALILI: Kuhisi hali ya kuwaka moto eneo chini ya kifua,kuhisi donge kooni kutokana na kutosagika kwa chakula na kusababisha kutofyonzwa vizuri hivyo kutoyeyuka vizuri tumboni na kusababisha mzunguko hasi'Retrogessive bowel circulation' na pia tumbo kujaa gesi,kukosa choo na hata vidonda vya tumbo. Kimaumbile vyakula na majimaji hutafunwa'mdomoni',husagwa,huyeyushwa na husharabiwa'tumboni na mfuko wa chakula'. Tatizo huzidi baada ya kula,wakati wa funga,ukijilaza nj kwa wajawazito. USHAURI:Epuka kula mlo wenye viungo vingi,mafuta,chumvi na sukari.
SHUKRANI KWA ABDULAZIZ MALIK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment