Monday, 6 July 2015

AFICHA MWILI WA MAREHE NDANI KWA MUDA WA SIKU SITA BILA YA WATU KUJUA

Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Biti Karo Mkazi wa Mkuranga, Kimanzichana Mtaa wa Makonde amefanya tukio la ajabu na la kushanga kwa jamii, mara baada ya kukaa na mwili wa marehemu Mama yake kwa muda wa siku sita ndani bila hata ndugu na majirani zake kufahamu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinasema Biti Karo alikuwa anakaa na Mama yake (Marehemu) akimuuguza.

Biti Karo aliyehusika kuuficha Mwili wa Marehemu
Chanzo chetu kinazidi kueleza kwamba, Majirani waliaanza kupata wasiwasi mara baada ya kutokumuona Mama huyo (Marehemu), kwani walikuwa wamemzoea akiwa nje na mwanae (Biti Karo) akiwa anampa dawa na chakula lakini ilipita siku kadhaa bila ya kumuona Mama huyo.
Majirani wakiwa kwenye eneo lililotokea msiba
Majirani walipoenda kumuulizia Biti Karo aliwajibu kwamba hajambo na yupo ndani amelala, lakini mnamo tarehe 4 july kijana mmoja alihisi harufu kali sana maeneo ya nyumba ya Biti Karo na alipojaribu kuuliza ni harufu ya nini, Biti Karo alijibu kwa kusema kwamba inawezekana ni harufu ya Panya.
Mwili wa Marehemu ukionekana kwa mbali
Mnamo siku ya jumapili july 5 Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Bibi Huruma ambaye ni ndugu wa Biti Karo alikwenda kuwatembelea na kumjulia hali mgonjwa, alipofika alishangaa kusikia harufu kali na alipouliza ni harufu ya kitu gani?, Biti Karo hakujibu kitu chochote.
Bibi Huruma alipoingia ndani alikuta Mama yao amefariki huku mwili wake ukitoa harufu na sehemu nyingine zikiwa zimechanika na kupasuka ndipo hapo alipopiga mayowe na majirani kusogea eneo hilo.
Majirani wote walishangaa kuona tukio hilo ambapo wengine walienda kumtaarifu Mjumbe aliyejulikana kwa jina la Kuisele, Mjumbe alimuita Mwenyekiti kisha wakawapigia simu Polisi.
Baada ya Polisi kufika na kuchukua maelezo waliamuru mwili wa marehemu kuzikwa.
Majirani wakiwa eneo la tukio
Chanzo chetu cha habari kinanaeleza kwamba mwili wa marehemu ulikuwa umeharibika sana na ilikuwa ngumu hata kuoshwa hivyo ulizikwa bila ya kuoshwa na wala kufanyiwa heshima yoyote.
Vijana wakiwa kwenye harakati ya kuchimba kaburi kwa ajili ya kuzika mwili wa Marehemu
Baada ya mwili wa marehemu kuzikwa Polisi waliondoka huku wakiwaacha wakazi wa eneo hilo kwenye hali ya kutofahamu nini kinaendelea kwani mpaka sasa Biti Karo yupo huru na wala haonyeshi hali ya kustushwa kwa kile kilichotokea.

1 comment:

Anonymous said...



aziz bilal6 juli 2015


1

Siwezi kushangaa na kushtushwa na biti karo kwa hatua aliyoamua kuichukua,inawezekana masuala ya kisaikologia ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kwa jinsi huyo binti alivyoamua kutotaka mtu yeyote ajue kifo cha mama yake mzazi,inavyoonekana huyo binti kapata maumivu makali sana ktk akili yake ambayo yamemfanya asitangaze kifo cha mama yake mzazi

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!