Saturday, 13 June 2015

WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA NGOZI KILA BAADA YA MIEZI MINNE

mail.google.com
……………………………………..
Watu wenye ulemavu wa ngozi wametakiwa kufanyiwa uchunguzi wa ngozi kila baada ya miezi Minne  ili kuepukana na saratani ya ngozi.


Hayo yamesemwa na meneja mpango wa kutunza watu wenye ualbino Dkt.Alfred Naburi kwenye viwanja vya shekhe Amri Abeid, wakati wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya siku ya ualbino duniani
Dkt.Naburi alisema watu wenye ulemavu wa ngozi wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa ngozi zao mara kwa mara kwa kuwa ngozi zao ni rahisi kuathiriwa na hivyo kusababisha kupata saratani hivyo kupunguza muda wao wa kuishi
“watu wenye ualbino wasipopata ushauri na kutunza ngozi vyema mara nyingi hawaishi zaidi ya miaka thelathini”alisema
Hatahivyo alisema licha ya kuishi miaka thelathini,ndani ya miaka Mitano ni rahisi kupata magonjwa ya ngozi endapo hawatopata kutunza ngozi zao vyema
Naye mwenyekiti wa chama cha watu wenye albinism wilaya ya Bagamoyo mwalimu Hamis Ngomero alitoa wito kwa jamii kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi kuweza kuwashauri na kuwapeleka kwenye vituo vinavyotoa huduma za kiuchunguzi ili waweze kupata ushauri wa utunzaji ngozi zao ili kukabiliana na saratani ya ngozi.
Mpango wa kutunza watu wenye albinism upo chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii katika hospitali ya KCMC inahudumia watu 250 wenye ulemavu wa ngozi kwenye mikoa ya Arusha,Tanga na Kilimanjaro.
Siku ya kimataifa ya watu wenye ualbino duniani huadhimishwa kila mwaka nchini Tanzania tarehe 13  Juni,mwaka huu inaadhimishwa kitaifa jijini Arusha.Mgeni rasmi wa maadhimisho haya atakua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete


Na.Catherine sungura,MoHSW,Arusha

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!