Monday, 1 June 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MKUTANO WA PILI WA DHARURA WA VIONGOZI WA EAC KUHUSU MGOGORO WA BURUNDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia)  nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba  wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano 
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano 
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari,  Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio 
Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke. 

....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Rais Museven akipita katikati ya  Gwaride la heshima. 
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Picha na Reginald Philip

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!