Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia kesi ya Mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu
Marijani Abdubakari Msoffe baada ya kupokea taarifa toka kwa
MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) , Biswalo Mganga Leo Kuwa Hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhoji wa na mtu yoyote wala mamlaka yoyote ile.
Hata hivyo dakika Chache baada ya Kufutiwa Kesi hiyo ya mauji kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 ambapo kisheria Mahakama ya Kisutu ilikuwa haina mamlaka ya kuisikiliza na haina dhamana na hivyo kwa Kipindi chote hicho tangu Agosti 10 Mwaka 2012 hadi Leo alikuwa akiishi Gereza la Keko Kisha aamishiwa gereza la Ukonga .
Leo pia upande wa Jamhuri umemfungulia Kesi mmoja ya kughushi Nyaraka za Viwanja ambayonendapo akitiiza Masharti ya dhamana anapata dhamana na hivyo kurudi nyumbani kwake kuungana na familia yake.
Hata hivyo hadi sasa bado hajatekeleza Masharti ya dhamana bado yupo chini ya Ulinzi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Pole Msoffe na hongera kwakufutiwa Kesi hiyo Ndio Sheria lazima ifutwe na wale waliopewa jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria.Na Imani kwa kupata tuhuma zile za Kesi za Mauji na kukasababisha ukaishi gerezani ni wazi utakuwa umejifunza sasa Kuwa Sheria zipo ,hazibagui masikini wa Tajiri wala Mtu maarufu,na dola linanguvu sana kuliko mwananchi wa aina yoyote yule na linamkono mrefu . Ushauri wangu jiepushe kukaribia au Kutenda mambo yanavunja Sheria.
Msoffe ambaye wewe ni shabiki mwenzangu wa Bendi ya FM academia nakushauri kaa mbali na tuhuma mbaya ambazo umekuwa ukisifika nazo sina haja ya kuzitaja hapa.
Nakumbuka Uliwahi kushitakiwa kwa Kesi Moja katika Mahakama ya Kisutu ukaenda Jela kwa kukosa dhamana na Kesi ile ikaisha ila Kesi hii ya Mauji ilisababisha licha na Umaarufu wako wote Ukaa Jela kwa Kipindi chote hicho.
Nimelazimika kuandika story hii ya Msoffe Kufutiwa Kesi hii Kwani Mimi nilikuwa ni miongoni mwa waandishi wa Habari tuliokuwa siku ya kwanza anafikishwa mahakamani hapo kuandika Habari yake mfululizo hadi baadhi ya ndugu zake wakawa wanatuzuia tusimpige picha na kututolea maneno machafu bila kujua tulikuwa tukitimiza wajibu wetu hadi nilipoachakazi ya uandishi wa habari katika gazeti la Tanzania Daima Agosti mwaka 2014 ndipo nilipoacha kuandika kesi hii.Tulishawasamehe.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
24/6/2015
Tujikumbushe habari niliyoiandika siku ya kwanza wakati Papa Msoffe alipofunguliwa Kesi hiyo ya Mauji ambayo Leo amefutiwatiwa na DPP.
10/8/2012
PAPA MSOFFE KORTINI KWA KESI YA MAUJI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya mauji. Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa m
oja la mauji ambalo ni kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Wakili Kweka alidai kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika. Kwa upande wake hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauji na mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote.
“Kwa sababu hiyo naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe gerezani”alisema Hakimu Mchome. Msofe ambaye alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao.
Msofe ambaye jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji.
Itakumbukwa hivi karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu. Aidha itakumbukwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Papa Msofe kufikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mbalimbali ya jinai.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Agosti 11 mwaka 2012
No comments:
Post a Comment