Ndugu zangu,
Leo nilipokuwa nikiongea na wanahabari pale Ukumbi wa Habari Maelezo, mbali ya mambo mengine kuhusu kipindi kipya cha ' Nyumbani Na Diaspora'. Nilizungumzia changamoto wanazozipata Watanzania hata kwenye kurudi nyumbani kwenye nchi waliyozaliwa.
Nilisema , kuwa kwa maoni yangu Uraia Pacha ni suala la wakati. Kuwa utakuja wakati tutakuja kujiuliza ilikuwaje tulitumia muda mwingi kujadili uraia pacha wakati ni kitu cha kawaida katika dunia ya sasa. Tutaziona faida zake.
Lakini, wakati umefika pia kubadilisha taratibu zetu. Ili Mtanzania aanze uwekazaji atahitaji kwenda sehemu tofauti na kwa wiki kadhaa kukamilisha taratibu. Ingewezekana kwenye jengo moja mtu akamaliza taratibu za Brela, TRA na nyinginezo katika kusajili biashara yake.
Na kwenye viwanja vyetu vya ndege?
Mpaka hii leo, bado mtu anajaza fomu kueleza madhumuni ya kurudi nyumbani!
Mpaka hii leo, bado mtu anajaza fomu kueleza madhumuni ya kurudi nyumbani!
Maggid
No comments:
Post a Comment