Friday, 26 June 2015

CHAKULA CHA MGONJWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

vidonda vya tumbo
Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo kisha tukasoma kuhusudawa mbadala ya vidonda vya tumbo na leo tunaendelea kuangalia chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.


Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji waasidi tumboni au mwilini kwa ujumla.
Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.
Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.
Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.
Mtu mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za majani. Anahitaji zaidiukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali.
Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10. Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].
Hapa chini nimekuwekea jedwali la jumla la vyakula na vinywaji vyenye asidi sana, asidi ya kati na alkalini sana, vile vya kuviepuka ni vile vyenye asidi sana, orodha itaendelea kuboreshwa;
Mayai na bidhaa za maziwa
  • Alkaline: mtindi
  • Neutral: mtindi mtupu (plain Yogurt ),
  • Acid: siagi, krimu, mayai, jibini ngumu (Hard Cheese), Ice Cream, jibini ya kiwandani (Processed Cheese), maziwa

Vyakula jamii ya maharage
  • Alkaline: Lima, njegere, Snap, String
  • Neutral: Soya
  • Acid: Black, Garbanzo, Kidney, dengu

Vyakula jamii ya karanga
  • Alkaline: lozi, Nazi freshi (fresh)
  • Neutral:
  • Acid: Brazil, korosho, Nazi kavu (dried coconut), Macadamia, karanga, Pecan, Pistachio, Walnut

Mboga za majani
  • Alkaline: asparaga (Asparagus), kiazisukari (Beets), brokoli (broccoli), kabeji, karoti, Koliflawa (aina ya kabichi – Cauliflower), figili (Celery), tango, mwani (Kelp), saladi (Lettuce), uyoga, vitunguu, kotimiri (Parsley), Bell Peppers, viazi ambavyo havijamenywa (with skin), boga (Squash), nyanya
  • Neutral: Horseradish, Rhubarb, Sauerkraut
  • Acid: Spinachi iliyopikwa, viazi ambavyo vimemenywa (no skin Potato), achali

Matunda
  • Alkaline: tufaa (Apple), parachichi, tende, mtini, zabibu, balungi, Kiwi, Limau, ndimu, embe, tikiti maji, chungwa, mpichi, Pears, Stroberi
  • Neutral:
  • Acid: Blueberry, Cranberry, plamu (Plum), plamu kavu (Prune)

Vinywaji
  • Alkaline: Maji ya limau, Chai ya tangawizi
  • Neutral: Maji
  • Acid: Chai ya rangi, Bia, kahawa, vinywaji vyenye kafeina, juisi za viwandani (processed), Liquor, Soda, Wine

Viongeza utamu
  • Alkaline: Asali mbichi (Raw Honey), sukari mbichi (Raw Sugar), Stevia
  • Neutral:
  • Acid: Viongeza utamu vyote vya kutengenezwa (Artificial Sweeteners)

Nyama
  • Alkaline:
  • Neutral:
  • Acid: Nyama ya ng’ombe, kuku, Samaki, mbuzi, batamzinga, nyama ya nguruwe, Sungura

Mafuta
  • Alkaline: mafuta ya mbegu za katani
  • Neutral: mafuta ya lozi, Canola, mafuta ya nazi, mafuta ya mahindi, Margarine, mafuta ya zeituni, Safflower, mafuta ya ufuta, mafuta ya Soya,mafuta ya alizeti
  • Acid:

Vitafunwa & nafaka
  • Alkaline: Amaranth, Millet, Quinoa
  • Neutral:
  • Acid: Barley, Buckwheat, Oats, mchele, Rye, Spelt, ngano, Pasta (vyakula jamii ya tambi), biskuti

Mbegu
  • Alkaline: Alfalfa (sprouted), chia (sprouted), Sesame (sprouted)
  • Neutral:
  • Acid: boga, alizeti, ngano
KWA HISANI YA FADHILI PAULO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!