
Zoezi la uandikishaji katika daftri la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa elektronia BVR wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera limeigia dosali baada ya kubainika kundi la wahamiaji haramu kutoka nchi ya Rwanda na Uganda wakijiandikisha kwa madai kuwa wamehamasishwa na wanasiasa kwa lengo la kupata wapiga kura.
Kata zilizokumbwa na mkasa wa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kata ya Kibingo inayopa kana na nchi ya Rwanda, kata ya Bugomora na kata ya Murongo zinazopakana na nchi ya Uganda ambapo wahamiaji haramu zaidi ya watu 50 wamekamatwa katika zoezi hilo huku afisa muandikishaji jimbo la Kyerwa Bw.George Mkindo akiwafukuza kazi waandishi wasaidizi kumi waliosajiliwa kuandikisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura baada ya kushindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuandikisha wahamiaji haramu kinyume cha sheria za uchaguzi.
Katika haliisiyokuwa ya kawaida mkazi wa kijiji cha Nyamiyaga ambaye anaishi na mhamiaji haramu kama mke wa ndoa na baadhi ya mwananchi wamesema kuwa wahamiaji haramu wamehamasishwa na wanasiasa huku wengine wakitishiwa kufukuzwa nchini endapo wasipojiandikisha kwenye daftari la kudum la wapiga kura.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.John Mongela ameipongeza kamati ya uandikishaji jimbo la Kyewa kwa kudhibiti wahamiaji haramu waliojipanga kupenyeza kujiandikisha katika daftari la kudumu ya wapiga kura na kusema kwamba serikali itaimarisha ulinzi katika maeneo ya mipaka ya nchi.













No comments:
Post a Comment