Friday, 1 May 2015

ALICHOSEMA RIDHWANI KIKWETE KUHUSU KUANGUKA KWA THAMANI YA SHILINGI




Nukuu toka kwa Wachumi
"Anguko la shilingi dhidi ya dola, japo ni anguko linaloonekana katika nchi nyingine dhidi ya dola vilevile na si kwetu pekee, sio jambo la kuchukulia kisiasa. Mbadilishano wa fedha (exchange rate) hujengwa na nguvu za uhitaji (demand) na zile za uuzaji (supply). Hizi ni nguvu za soko, sio nguvu za chama cha siasa wala serikali pekee, wala kikundi cha watu.

Uwekezaji zaidi katika kilimo na usindikaji utaleta ahueni. Tunahitaji pia bandari zaidi (moja tayari inajengwa Bagamoyo yenye uwezo-cargo handling: mara 20 ya bandari ya sasa ya Dar es Salaam), reli zaidi na barabara nzuri kuwezesha biashara ndani ya nchi na nchi jirani. Tunahitaji kuendelea kukuza uzalishaji wa bidhaa wa ndani.

Kwa Mtanzania wa kawaida anayetaka kusaidia shilingi kuwa imara dhidi ya fedha yoyote ya kigeni, kitu cha kwanza anachoweza kufanya kufanya ni kununua bidhaa zinazotengenezwa Tanzania kila zinapokuwepo (Play your part, rally behind the shilling, buy Made in Tanzania)."
Mwisho wa kunukuu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!