Monday, 27 April 2015

ZAIDI YA WATU 1000 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KWA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI NEPAL‏




Zaidi ya watu elfu moja wamepoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal karibu na mji mkuu wa Kathmandu.



Polisi wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakishindwa kujulikana walipo kwa hofu huenda wamefukiwa na kifusi.



Taarifa zinadai kuna uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara mji wa pili kwa ukubwa nchini Nepal. 



Tetetemeko hilo la ardhi ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 81 na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani kaskazini mwa India na Bangladesh. 



Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.



Naibu balozi wa Nepal mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa mamia ya watu wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa kila sehemu kubwa na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali ni nchi nzima imeathirika. 



Nepal ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo mwaka 1934 likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha yao.


Baadhi ya Waokoaji wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo aliekuwa amefukiwa kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma kutokana na tetemeoko hilo.


Sehemu ya athari za tetemeko hilo.


Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.


Wananchi wa Nepal wakishirikiana kwa pamoja kuvuta kamba. 




Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.

 

Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!