Friday 17 April 2015

BABA ASEMA YUKO TAYARI KUUZA FIGO ILI KUOKOA MAISHA YA WATOTO WAKE WENYE UZITO WAAJABU

(Kutoka kushoto) Yogita, mitano, Harsh, miezi 18, and Anisha, mitatu, (34kg), (15kg) na (48kg).
Baba maskini amedhihirisha mipango yake ya kuuza figo yake ili kuweza kuokoa maisha ya matibabu ya wanawe watatu wenye viriba tumbo (obese).
Wasichana Yogita Rameshbhai Nandwana, (5), na Anisha (3) na ndugu yao Harsh mwenye miezi 18, ni miongoni mwa watoto wazito duniani.
Wakiwa na kilo 34, kilo 48 na kilo 15, chakula wanachokula kwa wiki kinatosha kulisha familia mbili kwa mwezi.

Baba, mama pamoja watoto wao, wote wanaishi Gurjarat, India.
Sasa baba yao Rameshbhai Nandwana, 34, wa Gurjarat, India , anapanga kuuza figo yake kupata fedha ili awapeleke kwa mtaalamu.
Alisema: “Kama wanangu wataendelea kukua kwa kasi hii watakuwa na matatizo ya kiafya. Tunahofia watakufa.”
Yogita na Anisha hula chapatti 18, kilo 3 cha mchele, pakiti sita za krispsi, pakiti tano za biskuti, ndizi 12 na lita moja ya maziwa kila siku.
Chakula wanachokula watoto hao kwa wiki hulisha familia mbili kwa mwezi.
Na kwa kuwa wana njaa sana basi mama yao Pragna Ben, 30, hushinda akiwapikia chakula kutwa nzima.
Alisema: “Siku yangu huanza kwa kutengeneza chapatti 30 na kilo moja ya mboga za majani asubuhi, baada ya hapo naenda jikoni kuandaa chakula zaidi.
“Njaa zao haziishi, wanataka chakula muda wote na hulia na kupiga kelele kama hawalishwi. Muda wote niko jikoni nikiwapikia.”
Baba akiwa na wanae hao wenye viribatumbo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!