Sheria mpya nchini kenya kuanza kutumika kwa wafungwa wote wanaotumikia vifungo vyao kutopata chakula cha bure magerezani
Hayo yamesemwa na waziri wa usalama Joseph Nkaissery wa nchini kenya kwamba wafungwa hao wanatakiwa kuisaidia serikali katika kushiriki kwenye maswala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ili kupunguza gharama kubwa ambayo serikali inatumia kwa ajili ya kuwatunza.
Nkaissery anasema kwamba inakuwaje serikali itumie pesa nyingi kuwalisha watu waliovunja sheria na kuishia kufungwa, hivyo wanapaswa kuwa sehemu ya kuleta maendeleo ya Taifa na sio kuwahifadhi watu wanao liingiza taifa katika hasara.
No comments:
Post a Comment